Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kitabu cha Danieli Chashtakiwa
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • MTAWALA AMBAYE HAKUTAJWA

      7. (a) Kwa nini wachambuzi wa Biblia wamependezwa kwa muda mrefu na jinsi Danieli anavyomtaja Belshaza mara kadhaa? (b) Dhana ya kwamba Belshaza alikuwa mtu bandia ilipatwa na nini?

      7 Danieli aliandika kwamba Belshaza, “mwana” wa Nebukadreza, alikuwa akitawala Babiloni akiwa mfalme wakati jiji hilo lilipopinduliwa. (Danieli 5:1, 11, 18, 22, 30) Kwa muda mrefu, wachambuzi wameishambulia taarifa hiyo, kwa kuwa jina la Belshaza halikupatikana kwingineko isipokuwa katika Biblia. Badala yake, wanahistoria wa kale walimtambulisha Nabonido, mwandamizi wa Nebukadreza, kuwa mfalme wa mwisho wa Babiloni. Kwa hiyo, mwaka wa 1850, Ferdinand Hitzig alisema kwamba kwa wazi Belshaza alibuniwa na mwandikaji. Lakini, je, maoni ya Hitzig hayaonekani kuwa ya haraka-haraka tu? Je, kwani kukosa kutajwa popote kwa mfalme huyo—hasa wakati ambapo yakubalika kwamba rekodi za historia zilikuwa chache—kwa kweli kungethibitisha kwamba hakupata kuishi kamwe? Haidhuru, mwaka wa 1854 silinda kadhaa ndogo za udongo zilifukuliwa kwenye magofu ya Uru, jiji la Babiloni la kale, mahali ambapo sasa ni sehemu ya kusini ya Iraki. Hati hizo za kikabari za Mfalme Nabonido zilitia ndani sala kwa niaba ya “Bel-sar-ussur, mwanangu mkubwa.” Hata wachambuzi walilazimika kukubali: Huyo ndiye aliyekuwa Belshaza wa kitabu cha Danieli.

      8. Ufafanuzi wa Danieli kwamba Belshaza alikuwa mfalme anayetawala umethibitishwaje kuwa kweli?

      8 Hata hivyo, wachambuzi hawakuridhika. “Hilo halithibitishi jambo lolote,” akaandika mchambuzi mmoja aitwaye H. F. Talbot. Alidai kwamba huenda mwana huyo katika maandishi hayo alikuwa mtoto tu, ilhali Danieli amtaja kuwa mfalme anayetawala. Ingawa hivyo, mwaka mmoja tu baada ya maelezo ya Talbot kuchapishwa, mabamba mengine zaidi ya kikabari yaliyomrejezea Belshaza akiwa na waandishi na wafanyakazi wa nyumbani, yalifukuliwa. Bila shaka Belshaza huyo hakuwa mtoto! Hatimaye, mabamba mengine yakakata maneno, yakiripoti kwamba nyakati fulani Nabonido hakuweko Babiloni kwa miaka kadhaa. Mabamba hayo yalionyesha pia kwamba katika vipindi hivyo, “alimkabidhi ufalme” wa Babiloni mwanaye mkubwa (Belshaza). Nyakati hizo, Belshaza kwa kweli alikuwa mfalme—akitawala pamoja na baba yake.b

  • Kitabu cha Danieli Chashtakiwa
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • b Nabonido hakuweko Babiloni lilipoanguka. Kwa hiyo, Belshaza atajwa kwa kufaa kuwa mfalme wakati huo. Wachambuzi hubisha kwamba rekodi zisizo za kidini hazimtaji Belshaza kwa cheo rasmi cha mfalme. Hata hivyo, uthibitisho wa kale wadokeza kwamba siku hizo hata liwali angeweza kuitwa mfalme na watu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki