Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Baraka ya Yehova Juu ya “Nchi” Yetu
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Machi 1
    • 4, 5. Ni jinsi gani unabii wa Yoeli unaohusu mto unafanana na ule wa Ezekieli, na kwa nini hilo ni muhimu?

      4 Huenda unabii huo mzuri uliwakumbusha Wayahudi wahamishwa unabii mwingine uliorekodiwa zaidi ya karne mbili mapema: “Chemchemi itatokea katika nyumba ya BWANA, na kulinywesha bonde la Shitimu.”a (Yoeli 3:18) Unabii wa Yoeli, kama ulivyo wa Ezekieli, unatabiri kwamba mto ungetiririka kutoka kwenye nyumba ya Mungu, lile hekalu, na kutokeza uhai katika eneo la ukame.

      5 Kwa muda mrefu gazeti Mnara wa Mlinzi limeeleza kwamba unabii wa Yoeli unatimizwa siku zetu.b Kwa hakika basi, iko vivyo hivyo kwa habari ya ono la Ezekieli linalofanana na unabii huo. Katika nchi iliyorudishwa ya watu wa Mungu leo, kama tu katika Israeli la kale, baraka za Yehova zimetiririka kwelikweli.

  • Baraka ya Yehova Juu ya “Nchi” Yetu
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Machi 1
    • a Bonde hilo la mvo huenda larejezea Bonde la Kidroni, linaloenea kusini-mashariki mwa Yerusalemu na kuishia kwenye Bahari ya Chumvi. Sehemu ya chini ya bonde hilo ni kavu na yenye ukame mwaka mzima.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki