Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Tuambie, Mambo Haya Yatakuwa Wakati Gani?”
    Mnara wa Mlinzi—1994 | Februari 15
    • 11 Kama ilivyosimuliwa kwenye Matendo 2:1-4 na 14-21, katika Pentekoste 33 W.K., Mungu alimwaga roho takatifu juu ya wanafunzi 120, wanaume kwa wanawake. Mtume Petro alijulisha kwamba hayo ndiyo Yoeli alikuwa ametabiri. Hata hivyo, namna gani yale maneno ya Yoeli juu ya ‘jua kugeuzwa kuwa giza na mwezi kuwa damu na nyota kuacha kuangaza’? Hakuna lolote lionyeshalo kwamba hilo lilitimizwa katika 33 W.K. au katika kile kipindi cha zaidi ya miaka 30 cha umalizio wa mfumo wa mambo wa Kiyahudi.

      12, 13. Yale matukio ya kiajabu-ajabu ya kimbingu yaliyotabiriwa na Yoeli yalitimizwaje?

      12 Yaonekana sehemu hiyo ya mwisho ya utabiri wa Yoeli ilihusika kwa ukaribu zaidi na ‘kuja kwa siku ya Yehova iliyo kuu na itishayo’—kuharibiwa kwa Yerusalemu. Mnara wa Mlinzi la Desemba 1, 1967, lilisema hivi juu ya dhiki iliyopata Yerusalemu katika 70 W.K.: “Hiyo ikawa kweli kweli ‘siku ya Bwana’ kwa habari ya Yerusalemu na watoto wake. Na kuhusiana na siku hiyo kulikuwako ‘damu na moto, na mvuke wa moshi’ tele, jua lising’arishe giza zito la mji mchana, na mwezi ukionyesha damu iliyomwagika, isiwe mbalamwezi ya amani usiku.”c

      13 Naam, kama ilivyo katika ule unabii mwingine mbalimbali ambao tumeona, yale matukio ya kiajabu-ajabu ya kimbingu yaliyotabiriwa na Yoeli yangetimizwa wakati Yehova angetekeleza hukumu. Badala ya kuenea katika kipindi kizima cha umalizio wa mfumo wa Kiyahudi, kutiwa giza kwa jua, mwezi, na nyota kulitukia wakati majeshi yenye kufisha yalipokuja dhidi ya Yerusalemu. Kwa kufaa, twaweza kutazamia utimizo mkubwa zaidi wa sehemu hiyo ya unabii wa Yoeli wakati Yehova aanzapo kutekeleza hukumu dhidi ya mfumo wa sasa.

  • “Tuambie, Mambo Haya Yatakuwa Wakati Gani?”
    Mnara wa Mlinzi—1994 | Februari 15
    • c Yosefo aandika juu ya matukio kati ya shambulio la kwanza la jeshi la Waroma dhidi ya Yerusalemu (66 W.K.) na kuharibiwa kwalo: “Wakati wa usiku dhoruba yenye uharibifu mkubwa ilitokea; kimbunga kilipiga, mvua kubwa ajabu ilinyesha, umeme ulizidi kumweka, ngurumo zilikuwa zenye kuogofya, dunia ilitetemeka kwa mingurumo yenye kutia uziwi. Msiba kwa jamii ya kibinadamu ulitangulia kufananishwa waziwazi na mvunjiko huo wa muundo mzima wa mambo, na hakuna mtu angeweza kutia shaka kwamba ishara hizo zilimaanisha balaa isiyo na kifani.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki