-
Samaria—Jiji Kuu Miongoni mwa Majiji Makuu ya KaskaziniMnara wa Mlinzi—1990 | Novemba 1
-
-
Ingawa hivyo, baada ya miaka sita, Omri alifanyiza jiji kuu jipya. Wapi? Aliununua mlima ambao wauona upande wa kushoto, Samaria. (1 Wafalme 16:23-28) Ingawa sasa una matungazi mengi ya ukulima, yaelekea Omri aliuchagua kwa sababu kile kilima chenye kilele tambarare ambacho huchomoza kutoka kwenye uwanda kililindwa kwa urahisi. Mwana wake Ahabu aliendelea kujenga Samaria, kwa wazi akipanua maboma yalo kwa kuta zenye maki makubwa. Pia alijenga hekalu kwa ajili ya Baali na jumba la kifalme kwa ajili yake mwenyewe na mke wake Mfoinike, Yezebeli. Machimbuo yamefunua magofu ya jumba la kifalme la Ahabu, katika ukurasa ufuatao. Hilo jumba la kifalme lilijulikana kwa anasa na uovu wa kuzidi mno. (1 Wafalme 16:29-33) Wazia ukimwona nabii Eliya akipanda juu kwenda kwenye jiji hili na kuitembea ile barabara pana ya kwenda kwenye jumba la kifalme, huko akashutumu vikali uovu wa Ahabu wenye kumtegemea Baali.—1 Wafalme 17:1.
-