Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Alijifunza Kuwa Mwenye Rehema
    Mnara wa Mlinzi—2009 | Aprili 1
    • Mfalme pia alianza kumwogopa Mungu. Aliinuka kutoka kiti chake cha ufalme, akavua nguo zake za kifahari, akavaa nguo za magunia ambazo watu wake walikuwa wamevaa, na hata ‘akaketi katika majivu.’ Ingawa tayari watu wenyewe walikuwa wameanza kufunga, sasa mfalme pamoja na “wakubwa,” au watu wenye vyeo, alitoa agizo la kisheria kwamba watu wote wanapaswa kufunga. Aliamuru kwamba watu wote na pia wanyama wa kufugwa wavae nguo za magunia.c Alikiri kwa unyenyekevu kwamba watu wake walikuwa na hatia ya kutenda mabaya na jeuri. Pia alitumaini kwamba Mungu wa kweli angewaonyesha rehema alipoona kuwa wametubu. Mfalme huyo alisema: ‘Huenda Mungu wa kweli atageuka na kuacha hasira yake inayowaka, tusije tukaangamia.’—Yona 3:6-9.

  • Alijifunza Kuwa Mwenye Rehema
    Mnara wa Mlinzi—2009 | Aprili 1
    • c Huenda jambo hilo likashangaza, lakini lilitukia katika siku za kale. Mwanahistoria Mgiriki Herodoto alisema kwamba Waajemi wa kale waliomboleza kifo cha jenerali maarufu kwa kuhusisha wanyama wa kufugwa katika desturi za kuomboleza.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki