Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Acheni Upendo Wenu wa Kidugu Uendelee!
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Agosti 1
    • 5. Twajuaje kwamba Yehova ana hisia-mwenzi?

      5 Je, Yehova ana hisia-mwenzi kama hiyo? Bila shaka. Mathalani, twasoma hivi juu ya kuteseka kwa watu wake Israeli: “Katika mateso yao yote yeye aliteswa.” (Isaya 63:9) Yehova hakuona tu taabu zao; alikuwa na hisia kuelekea hao watu. Kiwango cha jinsi ahisivyo chatolewa kielezi na maneno ya Yehova mwenyewe kwa watu wake, yaliyorekodiwa kwenye Zekaria 2:8, BHN: “Anayewagusa nyinyi anagusa mboni ya jicho langu.”a Mwelezaji mmoja aonelea hivi kuhusu mstari huo: “Jicho ni mojawapo ya viungo vilivyo tata zaidi na vilivyo vyepesi kudhurika mwilini mwa binadamu; na mboni ya jicho—tundu ambalo kwalo nuru ya mbinguni huingia kwa minajili ya kuona—ndiyo sehemu nyetivu zaidi, na pia ya maana, ya kiungo hicho. Hakuna chochote kiwezacho kuwasilisha vizuri zaidi lile wazo la utunzaji mwororo ulio bora sana wa Yehova kwa watu anaowapenda.”

  • Acheni Upendo Wenu wa Kidugu Uendelee!
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Agosti 1
    • a Hapa tafsiri fulani zadokeza kwamba mtu anayegusa watu wa Mungu anagusa jicho la Israeli au hata lake mwenyewe, bali si la Mungu. Kosa hilo lilitokana na waandishi fulani wa enzi za kati ambao, katika jitihada zao zilizopotoka za kurekebisha mafungu ya maneno waliyoona kuwa hayahusiki, walibadili mstari huu. Kwa hiyo walizuia wingi wa hisia-mwenzi za kibinafsi za Yehova zisionekane.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki