-
Namna ya Kuimarisha Vifungo vya NdoaMnara wa Mlinzi—1993 | Agosti 15
-
-
Mafarisayo walibisha kwamba Musa alikuwa amefanya maandalizi ya talaka kwa kuagiza kwamba “hati ya talaka” itolewe. Yesu akawajibu hivi: “Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi. Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.”—Mathayo 19:3-9.
-
-
Namna ya Kuimarisha Vifungo vya NdoaMnara wa Mlinzi—1993 | Agosti 15
-
-
Uandalizi wa Sheria ya Kimusa
Kufikia wakati Sheria ya Kimusa ilipotolewa, mahusiano ya ndoa yalikuwa yamezorota sana kufikia hatua ambapo Yehova, kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya Waisraeli, alifanya uandalizi wa talaka. (Kumbukumbu la Torati 24:1) Mungu hakukusudia Waisraeli watumie vibaya sheria hiyo ili wataliki wake zao kwa sababu ya kasoro ndogo-ndogo, kama inavyoonekana wazi katika amri yake kwamba walipaswa kumpenda jirani yao kama nafsi zao. (Mambo ya Walawi 19:18) Hata kutoa hati ya talaka kulikuwa kizuizi kwa sababu, hatua moja ya kuandika hati hiyo ilikuwa kwamba, yule mume aliyetaka talaka angalipaswa awaendee wanaume wenye mamlaka ya haki, ambao wangalijaribu sana kupatanisha mambo. La, Mungu hakutoa sheria hiyo ili kusitawisha haki yoyote ya mtu kumtaliki mke wake “kwa kila sababu.”—Mathayo 19:3.
Hata hivyo, hatimaye Waisraeli walipuuza kusudi na maana halisi ya sheria, wakatumia kwa ubinafsi kifungu hicho cha maneno ili kutaliki kwa msingi wowote waliopenda. Kufikia karne ya tano K.W.K., walikuwa wakiwatenda wake wa ujana wao mambo ya hiana wakiwataliki kwa kila sababu. Yehova aliwaambia kwa uthabiti kwamba alichukia kutaliki. (Malaki 2:14-16) Hiyo ndiyo hali ambamo Yesu alilaumu talaka kama ilivyokuwa ikizoewa na Waisraeli katika siku yake.
-