Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Hizi Ndizo Siku za Mwisho!
    Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele
    • 2. Yesu aliulizwa swali gani na wanafunzi wake, naye alijibuje?

      2 Kwa kielelezo, fikiria jibu ambalo Yesu alitoa kwa baadhi ya maswali yaliyotokezwa na wanafunzi wake. Siku tatu kabla ya Yesu kufa, wao walimuuliza hivi: “Ni nini itakuwa ishara ya kuwapo kwako na ya umalizio wa mfumo wa mambo?”a (Mathayo 24:3, NW) Kwa kujibu, Yesu alisema juu ya matukio na hali hususa za ulimwengu ambazo zingeonyesha kwa wazi kwamba mfumo huu usiomwogopa Mungu ungekuwa umeingia siku zao za mwisho.

  • Hizi Ndizo Siku za Mwisho!
    Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele
    • a Biblia fulani-fulani hutumia neno “ulimwengu” badala ya “mfumo wa mambo.” Kamusi iitwayo Expository Dictionary of New Testament Words ya W. E. Vine, husema kwamba neno la Kigiriki ai·onʹ “humaanisha kipindi cha muda usio dhahiri, au wakati unaoonwa kwa kuhusiana na yale yanayotukia katika hicho kipindi.” Nayo kamusi iitwayo Greek and English Lexicon to the New Testament ya Parkhurst (ukurasa 17) hutia ndani usemi “mfumo huu wa mambo” katika kuzungumzia matumizi ya ai·oʹnes (kwa wingi) kwenye Waebrania 1:2. Kwa hiyo fasiri hii “mfumo wa mambo” inapatana na maandishi-awali ya awali ya Kigiriki.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki