Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wale Wanawali Wenye Hekima na Wapumbavu
    Mnara wa Mlinzi—1990 | Aprili 15
    • “Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki. Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao. Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika. Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie.”

      Mafuta yafananisha kile kinachowaendeleza Wakristo wakiwa wanaangaza wakiwa vimulikaji, yaani, Neno la Mungu lililovuviwa, ambalo wanashika sana, pamoja na roho takatifu, ambayo husaidia katika kuelewa Neno hilo. Mafuta hayo ya kiroho huwezesha wale wanawali wenye busara waangaze nuru katika kumkaribisha bwana-arusi wakati wa mwandamano wa kwenda kwenye karamu ya arusi. Lakini jamii ya wale wanawali wapumbavu haina ndani yao, katika vyombo vyao, yale mafuta ya kiroho yanayohita-jiwa. Kwa hiyo Yesu aeleza linalotukia:

  • Wale Wanawali Wenye Hekima na Wapumbavu
    Mnara wa Mlinzi—1990 | Aprili 15
    • Baada ya Kristo kuwasili katika Ufalme wake wa kimbingu, jamii ya wale wanawali wenye busara ya Wakristo wa kweli wapakwa-mafuta waliamuka kwenye pendeleo lao la kuangaza nuru katika ulimwengu huu uliotiwa giza katika kusifu Bwana-arusi aliyerudi. Lakini wale waliofananishwa na wale wanawali wapumbavu walikuwa hawako tayari kuandaa sifa hii ya kukaribisha. Kwa hiyo wakati ufikapo, Kristo hawafungulii mlango wa karamu ya arusi mbinguni. Yeye awaacha nje katika weusi wa usiku mzito zaidi ya wote wa ulimwengu, wakapotee na wafanya kazi wengine wote wa uasi-sheria. “Basi kesheni,” Yesu amalizia, “kwa sababu hamjui siku wala saa.” Mathayo 25:1-13.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki