-
Yehova Hupendezwa Sana na Utumishi Wako wa Nafsi YoteMnara wa Mlinzi—1997 | Oktoba 15
-
-
16. (a) Yesu alipataje kuchunguza mchango wa mjane maskini? (b) Sarafu za mjane zilikuwa za kiasi gani?
16 Siku kadhaa baadaye, Nisani 11, Yesu alitumia siku ndefu katika hekalu, ambapo mamlaka yake ilitiliwa shaka na alitokeza maswali yenye kutatanisha ya ghafula juu ya kodi, ufufuo, na mambo mengine. Aliwashutumu waandishi na Mafarisayo kwa ‘kuzinyafua nyumba za wajane,’ kati ya mambo mengine. (Marko 12:40) Kisha Yesu akaketi, ni dhahiri katika Ua wa Wanawake, ambapo, kulingana na mapokeo ya Kiyahudi, kulikuwa na masanduku 13 ya hazina. Aliketi hapo kwa muda fulani, akitazama kwa uangalifu watu walipokuwa wakitumbukiza michango yao. Watu wengi matajiri walikuja, labda wengine wakionekana kuwa wenye kujiona kuwa waadilifu, hata kwa majivuno. (Linganisha Mathayo 6:2.) Yesu akamkodolea macho mwanamke mmoja mahususi. Macho ya kawaida huenda ikawa yasingeona jambo lolote lenye kutokeza kumhusu yeye au zawadi yake. Lakini Yesu, ambaye aliweza kujua mioyo ya wengine, alijua kwamba alikuwa “mjane maskini.” Yeye alijua pia kiwango barabara cha zawadi yake—“sarafu ndogo mbili, zenye thamani ndogo sana.”b—Marko 12:41, 42.
-
-
Yehova Hupendezwa Sana na Utumishi Wako wa Nafsi YoteMnara wa Mlinzi—1997 | Oktoba 15
-
-
b Kila moja ya sarafu hizi ilikuwa leptoni, sarafu ndogo zaidi ya Kiyahudi iliyotumiwa wakati huo. Lepta mbili (moja ni leptoni, nyingi ni lepta) zilitoshana na sehemu moja ya 64 ya mshahara wa siku. Kulingana na Mathayo 10:29, kuwa na sarafu ya asarioni (inayolingana na lepta nane), mtu angeweza kununua shomoro wawili ambao walikuwa miongoni mwa ndege wa bei ya chini zaidi waliotumiwa kwa chakula na maskini. Kwa hiyo mjane huyo alikuwa maskini kwelikweli, kwa kuwa alikuwa na nusu tu ya kiasi cha kununua shomoro mmoja, ambacho hakingeweza kutosha hata mlo mmoja.
-