Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yesu Awatuma Wanafunzi 70
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Machi 1
    • ILIKUWA ni vuli ya mwaka wa 32 W.K. Ni miezi sita tu iliyobakia kabla ya kifo cha Yesu. Kwa sababu hiyo, ili kuharakisha kazi ya kuhubiri na kuwaongezea mazoezi zaidi baadhi ya wafuasi wake, aliwachagua wanafunzi 70 na “kuwatuma wawili-wawili kumtangulia kuingia katika kila jiji na mahali ambako yeye mwenyewe alikuwa akitaka kwenda.”—Luka 10:1.a

      Yesu aliwatuma wanafunzi wake “kumtangulia” ili watu waweze kuamua upesi zaidi ikiwa walimwunga mkono Mesiya au walimpinga wakati ambapo Yesu mwenyewe aliwasili baadaye. Lakini kwa nini aliwatuma “wawili-wawili”? Kwa wazi, ni ili kwamba wapate kutiana moyo walipokabili upinzani.

  • Yesu Awatuma Wanafunzi 70
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Machi 1
    • Mara nyingi, Mashahidi wa Yehova huonekana wakihubiri wawili-wawili. Je, mengi zaidi hayangetimizwa ikiwa kila mmoja wao angehubiri peke yake? Labda. Hata hivyo, Wakristo leo hutambua manufaa za kuhubiri sambamba na mwamini mwenzao. Hilo hutoa kadiri fulani ya kinga watoapo ushahidi katika maeneo hatari. Kuhubiri pamoja na mwenzi pia huwawezesha wapya zaidi kunufaika na ustadi wa wahubiri wa habari njema wenye uzoefu. Kwa kweli, wote wawili waweza kuchangia badilishano la kitia-moyo.—Mithali 27:17.

  • Yesu Awatuma Wanafunzi 70
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Machi 1
    • a Biblia fulani na hati za kale za Kigiriki husema kwamba Yesu aliwatuma wanafunzi “sabini na wawili.” Hata hivyo, kuna utegemezo mwingi wa hati juu ya tafsiri “sabini.” Tofauti hii ya kiufundi haipasi kutukengeusha fikira kutoka kwenye hoja kuu, kwamba Yesu alituma kikundi kikubwa cha wanafunzi wake kwenda kuhubiri.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki