Tamasha za Kutoka Lile Bara la Ahadi
“Ole Wako, Korazini”—Kwa Nini?
WEWE kwa uhakika hungetaka Mungu atangaze ole juu yako, au ungetaka? Basi, fikiria jinsi Wayahudi wa majiji matatu ya Galilaya wapaswa kuwa walihisi wakati Mwana na Hakimu wa Mungu alipopiga mbiu hivi:
“Ole wako, Korazini! Ole wako, Betesaida! Kwa sababu kama kazi za nguvu zingalifanyika ndani ya Tiro na Sidona zilizofanyika ndani yenu, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu. Lakini ninawaambia ninyi, Itakuwa kuvumilika kwa Tiro na Sidona siku ya hukumu kupita ninyi. Nawe Kapernaumu, . . . Utashushwa hata Hadeze.”—Mathayo 11:21-23, ZSB.
Tamasha iliyo juu inakaza fikira kwenye moja la majiji hayo—Korazini. Picha hii inaonekana pia kwenye Julai/Agosti katika 1989 Calendar of Jehovah’s Witnesses. Kwa kupendeza, maneno ya Yesu kwenye Mathayo 11:21-23 yamo katika programu ya usomaji wa Biblia wa Mashahidi wa Yehova katika Agosti. Basi, inatupasa tujue nini kuhusu Korazini?
Angalia mahali lilipokuwapo Korazini la kale. Unaweza kuona magofu yalo katika sehemu ya mbele ya picha hii ya kupigwa. Halafu, angalia miti iliyo katika ufuo wa pwani ya kaskazini ya Bahari ya Galilaya. Hapo ndipo Kapernaumu lilipokuwa, karibu kilometa 3 kutoka hapo. Umbali ambao picha hii ya hewani imepigiwa huenda ukadokeza kwamba huo ulikuwa mtandao wa ardhi tambarare, lakini kwa kweli Korazini imo katika vilima vilivyoinuka meta kama 270 juu ya ufuo wa bahari.
Pia tunasaidika kwa kujua kwamba Bethsaida ilikuwa karibu umbali uo huo kutoka Kapernaumu, kandokando ya ufuo wa bahari. Hivyo, kwa kuyasuta majiji haya matatu, Yesu alikuwa akikaza fikira zake zote juu ya eneo dogo lililozunguka kitovu cha utendaji wake katika Galilaya. (Mathayo 4:13; Marko 2:1; Luka 4:31) Kwa nini Yesu alitangaza ole juu yayo?
Yesu alitumia wakati mwingi pamoja na mitume katika eneo hili, naye alifanya hapa kazi nyingi za nguvu. Karibu na Bethsaida alilisha kimuujiza watu zaidi ya 5,000, na alimrudishia mwanamume kipofu nguvu za kuona. (Marko 8:22-25; Luka 9:10-17) Miongoni mwa miujiza aliyofanya katika Kapernaumu au karibu na hapo ulikuwa kuponya kivulana mgonjwa akiwa mbali, akaponya mwanamume aliyepagawa na roho waovu, akawezesha mtu aliyepooza atembee, na akafufua binti ya ofisa mmoja wa sinagogi. (Marko 2:1-12; 5:21-43; Luka 4:31-37; Yohana 4:46-54) Ingawa Biblia haitutajii wazi ni ‘kazi gani za nguvu’ zinazohusianishwa na Korazini, Mathayo 11:21 inaonyesha kwamba Yesu alifanya miujiza ndani au karibu na mahali hapa. Hata hivyo, watu wa hapo hawakutaka kuwa na imani kuwa ndiye Mesiya mwenye kuungwa mkono na Mungu.
Kwa kutazama tamasha iliyoonyeshwa hapa ya Yesu akifanya kazi za jinsi hiyo, huenda ukauliza kwamba, ‘Watu wa Korazini wangewezaje kukosa itikio jinsi hiyo?’ Labda kidokezi kimoja kinapatikana miongoni mwa mawe basalti ambayo wachimbuzi wa vitu vya kale wamechimbua miongoni mwa magofu haya, ambayo ni ya tangu karne ya tatu W.K. Mabakio haya ni kutia ndani sinagogi moja katika kitovu cha jiji na maeneo ya kukaliwa na watu yaliyo karibu. Michongo isiyo ya kikawaida ilikuwa imefanywa katika baadhi ya mawe hayo kutoka kwenye sinagogi. Ya kitu gani? Ya maumbo yaliyotokana na hadithi za Kigiriki za kubuniwa tu, kama vile Medusa aliye nyoka mwenye nywele-nywele, na sentauri, binadamu-nusu na farasi-nusu. Kwa kuwa dini ya Wayahudi ingalipaswa kupinga vikali michongo ya jinsi hiyo ya kuabudu sanamu, kwa nini viongozi wa Kiyahudi katika Korazini waliiruhusu iwe juu ya sinagogi lao?
Nadharia moja ni kwamba “huenda ikawa mtaa huo ulikuwa na kawaida ya kuelekea kuonyesha ukarimu kwa kukubalia mambo ya namna nyingi yafanyike humo,” hiyo ikimpa Yesu sababu ya kutumainia itikio jema katika jiji hilo.a Lakini ikiwa maumbo haya ya kuchongelewa yanadokeza kidogo juu ya mwelekeo fulani uliokuwako siku ya Yesu, ingeweza kuwa kwamba walio wengi katika Korazini hawakuhangaikia sana kumwabudu “Baba katika roho na kweli.” (Yohana 4:23) Walionyesha hivyo kwa kutomkubali kwao Mesiya mfanya miujiza.
Yesu alipowatuma wanafunzi 70, alitumia tena usemi wa kutia chumvi ili kukazia ukosefu wa itikio uliohusu Korazini, Bethsaida, na Kapernaumu. Ikiwa Wakorazini waliokuwa Wagalilaya kama Yesu na ambao walizoea kuona kazi zake za nguvu nyingi hawakuitikia kwa njia yenye kupendeleka, wanafunzi hawakupaswa kushangaa ikiwa wakaaji wa majiji fulani mengine walimohubiri hawakuwapokea.—Luka 10:10-15.
Kwa hiyo tunapoyafikiria magofu meusi yasiyo na uhai ya Korazini, inatupasa tuthamini moyoni onyo lililo wazi sana katika “ole” wa Yesu. Kutotubu, kutoitikia kazi ya Mungu inayofanywa na watu wake, kunaweza kupunguza ubora wa mtu na kumletea ukiwa wakati ujao.
[Maelezo ya Chini]
a The World of the Bible, Buku 5, ukurasa 44, kilichotangazwa kwa chapa na Educational Heritage (Turathi ya Kielimu), Inc., New York, 1959.
[Ramani katika ukurasa wa 16]
(Ona Mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Chorazin
Bethsaida
Capernaum
Sea of Galilee
Tiberias
[Ramani]
Pictorial Archive (Near Eastern History) Est. and Survey of Israel
[Picha katika ukurasa wa 17]
[Picha Ramani katika ukurasa wa 16]
Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.