Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wewe Humtii Nani—Mungu Au Wanadamu?
    Mnara wa Mlinzi—2005 | Desemba 15
    • 7. Kwa nini kazi ya kuhubiri iliwakasirisha wakuu wa makuhani?

      7 Azimio la mitume la kuendelea kuhubiri liliwakasirisha wakuu wa makuhani. Baadhi ya makuhani, kutia ndani Kayafa mwenyewe, walikuwa Masadukayo, ambao hawakuamini ufufuo. (Matendo 4:1, 2; 5:17) Hata hivyo, mitume waliendelea kusisitiza kwamba Yesu alikuwa amefufuliwa. Isitoshe, wakuu wengine wa makuhani walikuwa wamejitahidi sana kupata kibali cha watawala wa Roma. Kwenye kesi ya Yesu, Pilato alipowapa nafasi ya kumkubali Yesu kuwa mfalme wao, wakuu wa makuhani walimkataa kwa kupaaza sauti hivi: “Sisi hatuna mfalme ila Kaisari.” (Yohana 19:15)a Mitume hawakusisitiza tu kwamba Yesu alikuwa amefufuliwa lakini pia walifundisha kwamba, mbali na jina la Yesu, “hakuna jina lingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu ambalo kupitia hilo lazima sisi tupate kuokolewa.” (Matendo 2:36; 4:12) Makuhani waliogopa kwamba ikiwa watu wangemwona Yesu aliyefufuliwa kuwa Kiongozi wao, huenda Waroma wangekuja na labda viongozi wa Kiyahudi wangepoteza ‘mahali pao na taifa lao pia.’—Yohana 11:48.

  • Wewe Humtii Nani—Mungu Au Wanadamu?
    Mnara wa Mlinzi—2005 | Desemba 15
    • a “Kaisari” huyo ambaye wakuu wa makuhani walimwunga mkono hadharani katika pindi hiyo alikuwa Maliki Mroma Tiberio aliyedharauliwa na watu na aliyekuwa mnafiki na muuaji. Tiberio alijulikana pia kwa mazoea yake machafu ya ngono.—Danieli 11:15, 21.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki