-
Wanawake Wakristo Wastahili Heshima na StahaMnara wa Mlinzi—1995 | Julai 15
-
-
1, 2. (a) Mazungumzo ya Yesu pamoja na mwanamke Msamaria karibu na kisima yalichochea hangaiko jipi, na kwa nini? (Ona pia kielezi-chini.) (b) Kwa kuhubiri kwa mwanamke Msamaria, Yesu alionyesha nini?
ADHUHURI moja kuelekea mwisho wa 30 W.K., kwenye kisima cha kale karibu na jiji la Sikari, Yesu alifunua jinsi alivyohisi wanawake walipaswa kutendewa. Yeye alikuwa ametumia asubuhi hiyo akisafiri kupitia nchi yenye vilima-vilima ya Samaria naye akawasili kisimani akiwa amechoka, mwenye njaa, na mwenye kiu. Alipokuwa ameketi kando ya kisima, mwanamke Msamaria alikaribia ili kuchota maji. “Nipe maji ninywe,” Yesu akamwambia. Ni lazima mwanamke huyo awe alimkazia macho kwa mshangao. Mwanamke huyo akauliza: “Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria?” Baadaye, wanafunzi wake waliporudi kutoka kununua vyakula, wao walistaajabu, wakitaka kujua ni kwa nini Yesu alikuwa “akisema na mwanamke.”—Yohana 4:4-9, 27.
2 Ni nini kilichochochea swali la mwanamke huyo na kuhangaika kwa wanafunzi? Yeye alikuwa Msamaria, na Wayahudi hawakuwa na uhusiano na Wasamaria. (Yohana 8:48) Lakini ni wazi kwamba kulikuwa na sababu nyingine ya kuhangaika. Wakati huo, mapokeo ya kirabi yalizuia wanaume wasiongee na wanawake hadharani.a Hata hivyo, Yesu alihubiri waziwazi kwa mwanamke huyo mwenye moyo mweupe, hata akimfunulia kwamba yeye alikuwa ndiye Mesiya. (Yohana 4:25, 26) Hivyo Yesu alionyesha kwamba asingeongozwa na mapokeo yasiyo ya kimaandiko, kutia na yale yaliyoshusha wanawake. (Marko 7:9-13) Kinyume cha hilo, kwa yale aliyofanya na kwa yale aliyofundisha, Yesu alionyesha kwamba wanawake wapaswa kutendewa kwa heshima na staha.
-
-
Wanawake Wakristo Wastahili Heshima na StahaMnara wa Mlinzi—1995 | Julai 15
-
-
a The International Standard Bible Encyclopedia yaeleza hivi: “Wanawake hawakula pamoja na wageni wa kiume, na wanaume walizuiwa wasiongee na wanawake. . . . Mazungumzo pamoja na mwanamke katika mahali pa hadharani lilikuwa jambo la kuchukiza hasa.” Mishnah ya Kiyahudi, ulio mkusanyo wa mafundisho ya kirabi, ilishauri hivi: “Msiongee sana na wanawake. . . . Yeye aongeaye sana na wanawake ajiletea maovu na apuuza funzo la Sheria na mwishowe atarithi Gehena.”—Aboth 1:5.
-