Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ongeza Amani Yako Kupitia Maarifa Sahihi
    Mnara wa Mlinzi—1987 | Aprili 15
    • 6. Yesu Kristo alionyeshaje kwamba ile kazi ya kuhubiri ilikuwa ndiyo ya maana zaidi kwake?

      6 Kuwa na maarifa sahihi ya Yesu kunataka kuwa na “akili ya Kristo” na kumwiga. (1 Wakorintho 2:16, NW) Yesu alikuwa mtangazaji wa ukweli mwenye shauku. (Yohana 18:37) Roho yake yenye bidii nyingi ya kueneza evanjeli haikuzuiwa na chuki za kijamii zisizo na msingi. Ingawa Wayahudi wengine walichukia Wasamaria, yeye alimtolea ushuhuda mwanamke Msamaria kando ya kisima. Kwani, hata kuzungumza kwa muda mrefu na mwanamke ye yote hadharani huenda kulikunjiwa uso!a Lakini Yesu hakuruhusu hisia za kijamii zimzuie kutoa ushuhuda. Kazi ya Mungu ilikuwa yenye kuburudisha. Yeye alisema: “Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake.” Furaha ya kuona itikio la watu, kama yule mwanamke Msamaria na watu wengi wa mji wake, kulimtegemeza Yesu kama chakula. —Yohana 4:4-42; 8:48.

  • Ongeza Amani Yako Kupitia Maarifa Sahihi
    Mnara wa Mlinzi—1987 | Aprili 15
    • a Kulingana na Talmud, walimu wa kale walishauri hivi: “Acheni mtu ye yote asiongee na mwanamke katika barabara za mji.” Ikiwa desturi hii ilienea katika siku za Yesu, inaweza kuwa ndiyo sababu wanafunzi wake “wakastaajabu kwa sababu alikuwa akisema na mwanamke.”​—Yohana 4:27.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki