Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wewe ni Mwenye Thamani Machoni pa Mungu!
    Mnara wa Mlinzi—1995 | Aprili 1
    • 1. Mtazamo wa Yesu kuelekea watu wa kawaida wa siku yake ulitofautianaje na ule wa Mafarisayo?

      WALIWEZA kuiona machoni pake. Mtu huyu, Yesu, hakuwa hata kidogo kama viongozi wao wa kidini; yeye alijali. Yeye aliwahurumia watu hawa kwa sababu “walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji.” (Mathayo 9:36) Viongozi wao wa kidini walitakiwa wawe wachungaji wenye upendo wakimwakilisha Mungu mwenye upendo, mwenye rehema. Badala ya hivyo, waliwadharau watu wa kawaida kuwa ovyo—na walaaniwa!a (Yohana 7:47-49; linganisha Ezekieli 34:4.) Kwa wazi, maoni hayo yaliyopotoka, yasiyo ya kimaandiko yalikuwa tofauti sana na maoni ya Yehova juu ya watu wake. Yeye alikuwa ameliambia taifa lake, Israeli: “Nimekupenda kwa upendo wa milele.”—Yeremia 31:3.

  • Wewe ni Mwenye Thamani Machoni pa Mungu!
    Mnara wa Mlinzi—1995 | Aprili 1
    • a Kwa kweli, wao waliwapuuza maskini kwa kutumia ule mtajo “ʽam-ha·ʼaʹrets,” au “watu wa ardhi.” Kulingana na msomi mmoja, Mafarisayo walifundisha kwamba mtu hakupaswa wala kutumaini watu hao na vitu vya kimwili, wala kutumaini ushuhuda wao, wala kuwakaribisha kuwa wageni wao, wala kuwa wageni wao, wala hata kununua vitu kutoka kwao. Viongozi wa kidini walisema kwamba kwa binti ya mtu kuolewa na mmoja wa watu hao kungekuwa kama kumfunua kwa hayawani-mwitu akiwa amefungwa na akiwa hoi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki