Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mamilioni Walio Wafu Sasa Wataishi Tena
    Mnara wa Mlinzi—1990 | Mei 1
    • Itikio la Yesu kwa kifo cha Lazaro hufunua upande wenye huruma nyororo sana wa Mwana wa Mungu. Hisia zake za kina kirefu katika pindi hii huonyesha wazi tamaa yake kubwa sana kufufua wafu. Twasoma hivi: “Mariamu alipofika pale alipokuwapo Yesu, na kumwona, alianguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake, akasema, Mmemweka wapi? Wakamwambia, Bwana, njoo utazame. Yesu akalia machozi. Basi Wayahudi wakasema, Angalieni jinsi alivyompenda.”—Yohana 11:32-36.

  • Mamilioni Walio Wafu Sasa Wataishi Tena
    Mnara wa Mlinzi—1990 | Mei 1
    • Usemi uliotafsiriwa “akafadhaika” watokana na neno la Kigiriki (ta·rasʹso) ambalo huonyesha mtetemeko. Kulingana na The New Thayer’s Greek-English Lexicon of the New Testament, hiyo humaanisha “kusababishia mtu msukosuko wa ndani, . . . kuathiri kwa umivu kubwa au majonzi.” Usemi “akalia machozi” hutokana na kitenzi cha Kigiriki (da·kryʹo) ambacho humaanisha “kumwaga machozi, kutoa machozi kwa unyamavu.” Hiyo yatofautiana na “kulia machozi” kwa Mariamu na Wayahudi waliokuwa pamoja naye, ambako kwatajwa kwenye Yohana 11:33. Hapo neno la Kigiriki (kutokana na klaiʹo) lililotumiwa humaanisha kulia machozi kwa njia yenye kusikika au kwa sauti kubwa.d

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki