-
“Hajasema Kamwe Mtu Mwingine Kama Hivi”Mnara wa Mlinzi—2002 | Septemba 1
-
-
6. Toa mfano unaoonyesha jinsi Yesu alivyotaja mambo muhimu sana kwa kutumia maneno machache.
6 Mara nyingi Yesu alitaja mambo muhimu sana kwa kutumia maneno machache, yaliyo wazi na rahisi. Ona mifano kadhaa: “Hakuna awezaye kutumikia kama mtumwa mabwana-wakubwa wawili; . . . hamwezi kutumikia kama watumwa Mungu na Utajiri.” “Komeni kuhukumu ili msipate kuhukumiwa.” “Kwa matunda yao mtawatambua watu hao.” “Watu wenye afya hawahitaji tabibu, bali wenye kuugua wahitaji.” “Wote wauchukuao upanga wataangamia kwa upanga.” “Mlipeni Kaisari vitu vya Kaisari, lakini mlipeni Mungu vitu vya Mungu.” “Kuna furaha zaidi katika kutoa kuliko kulivyo katika kupokea.”c (Mathayo 6:24; 7:1, 20; 9:12; 26:52; Marko 12:17; Matendo 20:35) Leo maneno hayo yangali yanakumbukwa ingawa Yesu aliyasema karibu miaka 2,000 iliyopita.
-
-
“Hajasema Kamwe Mtu Mwingine Kama Hivi”Mnara wa Mlinzi—2002 | Septemba 1
-
-
c Nukuu hili la mwisho linalopatikana katika andiko la Matendo 20:35, limenukuliwa na mtume Paulo peke yake, ijapokuwa maana ya maneno hayo imedokezwa katika vitabu vya Injili. Huenda Paulo alipokea maneno hayo kwa mdomo (ama kutoka kwa mwanafunzi fulani aliyemsikia Yesu akisema maneno hayo au kutoka kwa Yesu aliyefufuliwa) au kwa kufunuliwa na Mungu.—Matendo 22:6-15; 1 Wakorintho 15:6, 8.
-