Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ‘Kufahamu Sisi Ni Nini Wakati wa Ukumbusho’
    Mnara wa Mlinzi—1990 | Februari 15
    • 3 “Bwana Yesu katika usiku ambamo yeye alikuwa akienda kutolewa alichukua mkate na, baada ya kutoa shukrani, akauvunja na kusema: ‘Huu humaanisha mwili wangu ambao ni kwa ajili yenu. Fulizeni kufanya hivi kwa kukumbuka mimi.’ Alifanya hivyo hivyo kwa habari ya kikombe pia, baada ya yeye kwisha kuwa na mlo wa jioni, akisema: ‘Kikombe hiki humaanisha agano jipya kwa nguvu za damu yangu. Fulizeni kufanya hivi, mara nyingi nyinyi mnapokinywa, kwa kukumbuka mimi.’ Kwa maana mara nyingi nyinyi mnapokula mkate huu na mnapokunywa kikombe hiki, mwafuliza kupiga mbiu juu ya kifo cha Bwana, mpaka yeye awasili.”—1 Wakorintho 11:23-26, NWa

  • ‘Kufahamu Sisi Ni Nini Wakati wa Ukumbusho’
    Mnara wa Mlinzi—1990 | Februari 15
    • 3 “Bwana Yesu katika usiku ambamo yeye alikuwa akienda kutolewa alichukua mkate na, baada ya kutoa shukrani, akauvunja na kusema: ‘Huu humaanisha mwili wangu ambao ni kwa ajili yenu. Fulizeni kufanya hivi kwa kukumbuka mimi.’ Alifanya hivyo hivyo kwa habari ya kikombe pia, baada ya yeye kwisha kuwa na mlo wa jioni, akisema: ‘Kikombe hiki humaanisha agano jipya kwa nguvu za damu yangu. Fulizeni kufanya hivi, mara nyingi nyinyi mnapokinywa, kwa kukumbuka mimi.’ Kwa maana mara nyingi nyinyi mnapokula mkate huu na mnapokunywa kikombe hiki, mwafuliza kupiga mbiu juu ya kifo cha Bwana, mpaka yeye awasili.”—1 Wakorintho 11:23-26, NWa

  • ‘Kufahamu Sisi Ni Nini Wakati wa Ukumbusho’
    Mnara wa Mlinzi—1990 | Februari 15
    • “Huu Humaanisha Mwili Wangu”

      5, 6. (a) Yesu alifanya nini na mkate? (b) Alitumia mkate wa namna gani?

      5 Tumesoma mambo ambayo Paulo ‘alipokea kutoka kwa Bwana’ kwa habari ya Ukumbusho. Pia kuna masimulizi yaliyofanywa na waandikaji watatu wa Gospeli, mmoja akiwapo wakati Yesu alipoanzisha mwadhimisho huu. (1 Wakorintho 11:23, NW; Mathayo 26:26-29; Marko 14:22-25; Luka 22: 19, 20) Masimulizi haya yasema kwamba kwanza Yesu alichukua mkate, akasali, halafu akauvunja na kuugawanya. Mkate huo ulikuwa nini? Kwa ulinganifu, huo ni nini leo? Wamaanisha au wawakilisha nini?

      6 Hapo vilikuwapo vitu vilivyotokana na mlo wa Sikukuu-Kupitwa ya Kiyahudi, kimoja kikiwa ni mkate usio na hamira, ambao Musa aliuita “keki zisizochachwa, mkate wa mteseko.” (Kumbukumbu 16:3; Kutoka 12:8, NW) Mkate huu ulifanyizwa kwa unga-ngano bila kutumia hamira, chumvi, au vikolezo. Kwa kuwa haukutiwa hamira (Kiebrania, mats·tsahʹ). ulikuwa bapa na kuweza kuvunjika kwa urahisi; ilikuwa lazima uvunjwe kwa kiasi cha kulika.—Marko 6:41; 8:6; Matendo 27:35.

      7. Mashahidi wa Yehova hutumia nini kwa mkate wakati wa Ukumbusho?

      7 Yesu alitumia mkate usiotiwa hamira katika Mlo wa Jioni wa Bwana, na ndivyo wafanyavyo Mashahidi wa Yehova leo. Matzothi ambazo hutumiwa kwa ukawaida na Wayahudi zaweza kutumiwa kwa kusudi hili ikiwa hazikufanyizwa kwa kuongezewa vichanganyo vingine, kama kimea, vitunguu, au mayai. (Matzothi zenye viongezeo hivyo hazingelingana na lile elezo la “mkate wa mteseko.”) Au wazee wa kundi wangeweza kuagiza mtu fulani afanyize mkate usiotiwa hamira kutokana na mkando wa unga-ngano. na maji. Ikiwa unga-ngano haupo, mkate usiotiwa hamira waweza kufanyizwa kwa unga wa shayiri, mchele, mahindi, au nafaka nyingine. Mkando huo huviringwa-viringwa ukawa mwembamba na kuokwa juu ya kikaangio kilichotiwa mafuta ya kugusia-gusia tu.

      8. Kwa nini mkate usiotiwa hamira ni kifananishi kifaacho, na kuushiriki kwamaanisha nini? (Waebrania 10:5-7; 1 Petro 4:1)

      8 Mkate huo wafaa kwa sababu hauna hamira, ambayo Biblia yatumia kuwakilisha ufisadi au dhambi. Paulo alishauri hivi kuhusu mwanamume asiyefuata adili katika kundi moja: ‘Hamira kidogo huchachisha donge zima. Ondoleeni mbali ile hamira ya zamani, kwamba nyinyi mpate kuwa huru bila mchacho. Kristo sikukuu-kupitwa yetu amedhabihiwa. Acheni tuushike msherehekeo, si kwa hamira ya ubaya na uovu, bali kwa keki zisizochachwa za weupe wa moyo na ukweli.’ (1 Wakorintho 5:6-8, NW; linganisha Mathayo 13:33; 16:6, 12.) Mkate usiotiwa hamira ni kifananishi kinachofaa cha mwili wa Yesu wa kibinadamu, kwa maana yeye alikuwa “mwaminifu-mshikamanifu, asiye na hila, asiyetiwa unajisi, mwenye kutenganishwa na watenda dhambi.” (Waebrania 7:26, NW) Yesu alikuwapo akiwa katika mwili wake mkamilifu wa kibinadamu aliposema hivi kwa mitume: “Chukueni na kula [mkate] huu, wamaanisha mwili wangu.” (Mathayo 26:26, A New Translation of the Bible, ya James Moffatt) Kushiriki mkate kwamaanisha kwamba mtu huitikadi katika manufaa ya dhabihu ya Yesu kwa ajili yake na kuipokea. Ingawa hivyo, mengi zaidi yahusishwa.

  • ‘Kufahamu Sisi Ni Nini Wakati wa Ukumbusho’
    Mnara wa Mlinzi—1990 | Februari 15
    • a “Katika usiku ambao Yeye alitolewa, Bwana Yesu alichukua mkate; akitoa shukrani, Yeye akauvunja na kusema: ‘Huu ni mwili wangu ambao ni kwa ajili ya nyinyi; fanyeni hivi kuwa ukumbusho wangu.’ Vivyo hivyo Yeye alichukua kikombe wakati chajio kilipokwisha, akasema: ‘Kikombe hiki ndilo agano jipya, lenye kutiwa muhuri kwa damu yangu; kila wakati mkinywapo, fanyeni hivyo kuwa ukumbusho wangu.’”—An Expanded Paraphrase of the Epistles of Paul, ya F. F. Bruce.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki