Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w88 11/1 uku. 14
  • ‘Shaba Inayolia au Upatu Unaovuma’

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • ‘Shaba Inayolia au Upatu Unaovuma’
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Habari Zinazolingana
  • Upendo Ni wa Maana Sana
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • Fuateni Njia ya Upendo Ipitayo Zote
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Ufunguo wa Kupata Dini ya Kweli
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Upendo katika Matendo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1979
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
w88 11/1 uku. 14

‘Shaba Inayolia au Upatu Unaovuma’

Nani atakaye kuwa kelele kubwa tu isiyofaa kitu? “Kama sina upendo,” anasema mtume Paulo, “nimekuwa [kipande cha, NW] shaba iliayo na upatu uvumao [toazi ambalo linagonga kwa kishindo, NW].” (1 Wakorintho 13:1) Paulo alikuwa ametoka tu kukazia uhitaji wa kutumia zawadi za pekee zilizopokewa kupitia roho ya Mungu kwa manufaa ya kundi zima la Kikristo. Ikiwa upendo ungekuwa umekosekana, kiburi na ufidhuli ni mambo ambayo yangeweza kusababisha Mkristo awe kama kelele kubwa yenye kufanya kishindo, yenye kuziba masikio, ambayo ingeondosha wengine wasitake kuisikia badala ya kuwavutia.​—Ona 1 Wakorintho 12:4-9, 19-26.

Sisi huelewa kwa urahisi lile wazo la toazi ambalo linavuma karibu nasi, lakini namna gani juu ya kielezi kile kingine cha Paulo, ‘kipande cha shaba iliayo’? (Kigiriki, khal.kos’ e.khon’) Watu fulani wamefasiri neno hilo kuwa “upatu wenye makelele” (Today’s English Version) na “upatu unaolilisha-lilisha miangwi” (New International Version). William Harris, akiandika katika Biblical Archaeology Review, anaonyesha wazi kwamba e.khon’ linatokana na mzizi ule ule kama neno la Kiingereza “echo” (mwangwi), na kwa sababu hiyo likatokea lile wazo la kufanya mwangwi au kulilisha-lilisha miangwi. Hata hivyo, yeye anasema hivi pia: “Nomino chalkos inatumiwa kueleza vitu vingi vya namna mbalimbali vya kuyeyushwa katika kalibu ambavyo vinatokana na mchanganyiko wa shaba na bati unaoitwa bronzi au brasi​—silaha za vita, visu, magudulia, vioo, pesa, hata tableti. Lakini hakuna uthibitisho wa kwamba neno hilo lilitumiwa kwa chombo cha kimuziki.” Basi, ni dokezo gani alilo nalo?

Yeye anarejeza kwenye kitabu kimoja kilichotungwa na Vitruvius, stadi wa ramani za ujenzi aliyeishi katika karne ya kwanza K.W.K. Vitruvius aliandika juu ya tatizo la kufikisha sauti mbali katika majumba ya miigizo yaliyojengwa kwa vifaa kama marimari na akasema kwamba vitu maalumu vya kurudisha mwangwi vilitumiwa ambavyo viliitwa e.khei’a. Hivyo vilikuwa vyungu vilivyofanyizwa kwa bronzi na kupangwa nyuma ya jumba-mviringo la miigizo lililo kubwa sana ili kusaidia kukuza na kurusha mbali mlio wenye kutokezwa. Baadhi ya vitu hivyo vililetwa Roma kutoka jumba la miigizo lililoachishwa matumizi katika Korintho karibu miaka mia moja kabla ya Paulo kuandika barua yake kwa kundi la Korintho.

Tunaambiwa kwamba Plato alinena habari za chungu kimoja cha bronzi kilichozidi na kuzidi kuvumisha mwangwi, kama walivyofanya wanenaji fulani wenye vichwa vitupu. Hiyo inaafikiana na ule msemo wa Shakespeare kwamba “chombo kitupu ndicho hufanya mlio mkubwa zaidi” (debe tupu haliachi kuvuma). Ingeweza kuwa Paulo alikuwa na wazo kama hilo aliponena juu ya wale waliotumia sana zawadi zao maalumu lakini wakawa hawana ile zawadi kubwa kupita zote​—upendo. Wao walitokeza mwangwi kwa sauti kubwa lakini hawakuwa watu wenye umaana halisi. Wao walikuwa kama kelele kali-kali isiyo na upatano, badala ya kuwa mlio wenye kuvutia, wenye kusihi. Namna gani wewe? Je! vitendo na uneni wako vinasukumwa na upendo, au wewe ni ‘shaba inayolia au upatu unaovuma’?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki