Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ‘Kuendelea Kuangalia’ Masilahi za Watu Wazee-Wazee
    Mnara wa Mlinzi—1987 | Juni 1
    • 6, 7, na maelezo yaliyo chini. (a) ‘Kuandikwa katika orodha’ kulikuwa nini? (b) Kwa sababu gani wale ambao walikuwa chini ya umri wa miaka 60 walikosa kupokea tegemezo hilo? (b) Paulo alizuiaje wajane vijana wasipokee “hukumu” kali?

      6 Ndipo Paulo akasema: “Mjane asiandikwe [kati ya wale wenye kupokea tegemezo la kifedha] isipokuwa umri wake amepata miaka sitini.” Katika siku za Paulo mwanamke aliyekuwa na umri zaidi ya 60 kwa wazi alionwa kuwa hawezi kujitegemeza mwenyewea na haikuelekea kwamba wangeolewa tena. “Kwa upande ule mwingine,” Paulo akaagiza, “uwakatalie wajane wenye umri mdogo [wasiandikwe katika orodha] kwa maana wakati nyege zao zimekuja kati yao na Kristo, wao wanataka kuolewa, wakiwa na hukumu kwa sababu wamepuuza wonyesho wao wa kwanza wa imani.”​—1 Timotheo 5Mistari 9, 11, 12, NW.

  • ‘Kuendelea Kuangalia’ Masilahi za Watu Wazee-Wazee
    Mnara wa Mlinzi—1987 | Juni 1
    • a Walawi 27:1-7 linataja umri wa miaka 60 linapozungumza juu ya watu mmoja mmoja ‘waliotolewa kama mchango’ hekaluni (kwa kufanya nadhiri) wawe wafanya kazi. Bei ya kukombolewa ilitofautiana kulingana na umri. Kwenye umri wa miaka 60 bei hiyo ilianguka sana, inaonekana kwa sababu mtu mzee hivyo alionwa kuwa asiyeweza kufanya kazi kwa nguvu kama mtu mwenye umri mdogo. The Encyclopedia Judaica inaongezea hivi: “Kulingana na Talmudi, uzee . . . unaanzia miaka 60.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki