Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ‘Fanyeni Pigano Kali kwa Ajili ya Imani’!
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Juni 1
    • 5. Yuda anukuu kutoka nabii yupi wa kale, na unabii huo ulielezaje uhakika kamili wa utimizo wake?

      5 Baadaye, Yuda ataja hata hukumu yenye matokeo makubwa zaidi. Yeye anukuu unabii wa Enoki—kifungu kisichopatikana penginepo katika Maandiko yaliyopuliziwa.a (Yuda 14, 15) Enoki alitabiri wakati ambapo Yehova angehukumu watu wote wasiomwogopa Mungu na matendo yao yasiyo ya kumwogopa Mungu. Kwa kupendeza, Enoki alisema kwa kutumia kitenzi cha wakati uliopita, kwa kuwa hukumu za Mungu zilikuwa za hakika kana kwamba zilikuwa tayari zimetukia. Huenda ikawa watu walimdhihaki Enoki na baadaye Noa, lakini wadhihaki hao wote walikufa maji katika Gharika ya tufeni pote.

  • ‘Fanyeni Pigano Kali kwa Ajili ya Imani’!
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Juni 1
    • a Watafiti fulani husisitiza kwamba Yuda ananukuu kutoka katika kichapo cha kubuniwa kiitwacho Book of Enoch. Hata hivyo, R. C. H. Lenski aandika: “Twauliza: ‘Ni nini chanzo cha habari zilizokusanywa kufanyiza kichapo hiki, yaani Book of Enoch?’ Kitabu hiki ni tokeo la habari zilizoongezwa, na hakuna aliye na hakika juu ya tarehe za sehemu zake mbalimbali . . . ; hakuna awezaye kuwa na hakika kwamba baadhi ya maelezo yake labda, hayakutolewa kwa Yuda mwenyewe.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki