Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jiji Lenye Uzuri wa Kung’aa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 19. (a) Yohana huelezaje Yerusalemu Jipya likiwasilisha baraka kwa aina ya binadamu? (b) “Mto wa maji ya uhai” hutiririka lini, na twajuaje?

      19 Lile jiji lenye uzuri wa kung’aa litawasilisha baraka tukufu kwa aina ya binadamu duniani. Hilo ndilo Yohana anafuata kujifunza: “Na yeye akanionyesha mto wa maji ya uhai, mwangavu kama fuwele ukitiririka nje kutoka kiti cha ufalme cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kuteremka chini katikati ya njia pana yalo.” (Ufunuo 22:1, 2a, NW) “Mto” huu hutiririka lini? Kwa kuwa huo hutiririka “nje kutoka kiti cha ufalme cha Mungu na cha Mwana-Kondoo,” hiyo ingeweza kuwa tu baada ya siku ya Bwana kuanza katika 1914. Huo ndio uliokuwa wakati wa lile tukio lililotolewa habari kwa kupulizwa kwa tarumbeta ya saba na tangazo tukufu: “Sasa kumetukia wokovu na nguvu na ufalme wa Mungu wetu na mamlaka ya Kristo wake.” (Ufunuo 11:15; 12:10, NW) Katika nyakati za mwisho, roho na bibi-arusi wamekuwa wakiwaalika watu wenye mwelekeo unaofaa wanywe maji ya uhai bure. Maji ya mto huo yataendelea kupatikana kwa ajili ya watu kama hao mpaka mwisho wa mfumo huu wa mambo na, baadaye kuendelea katika ulimwengu mpya, wakati Yerusalemu Jipya ‘linapokuja chini kutoka katika mbingu kutoka kwa Mungu.’—Ufunuo 21:2, NW.

  • Jiji Lenye Uzuri wa Kung’aa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 23. (a) Ni kwa nini inafaa kwamba mto wa maji ya uhai hutiririka kupitia njia pana ya Yerusalemu Jipya? (b) Ni ahadi gani ya kimungu aliyopewa Abrahamu itatimizwa wakati maji ya uhai yatatiririka kwa utele?

      23 Wakati wa Utawala wa Miaka Elfu, manufaa za ule ukombozi zitatumiwa kikamili kupitia ukuhani wa Yesu na makuhani walio chini yake 144,000. Kwa kufaa, basi, mto wa maji ya uhai hutiririka kupitia katikati ya njia pana ya Yerusalemu Jipya. Walio washiriki walo ni Israeli wa kiroho, ambao pamoja na Yesu hujumlika kuwa mbegu ya kweli ya Abrahamu. (Wagalatia 3:16, 29) Kwa hiyo, maji ya uhai yanapotiririka kwa utele kupitia katikati ya njia pana ya jiji la ufananisho, “mataifa yote ya dunia” yatapata fursa kamili ya kujibarikia yenyewe kwa njia ya mbegu ya Abrahamu. Ahadi ya Yehova kwa Abrahamu itatimizwa kikamili.—Mwanzo 22:17, 18.

      Miti ya Uhai

      24. Yohana anaona nini sasa katika pande zote mbili za mto wa maji ya uhai, nayo ni picha ya nini?

      24 Katika njozi ya Ezekieli, mto hata ukawa mvo, na nabii akaona ikikua katika pande zao zote mbili namna zote za miti yenye kuzaa matunda. (Ezekieli 47:12) Lakini Yohana anaona nini? Hili: “Na upande huu wa mto na upande ule kulikuwa na miti ya uhai ikifanyiza mazao kumi na mawili ya tunda, ikitoa matunda yayo kila mwezi. Na majani ya miti yalikuwa kwa ajili ya kuponeshwa kwa mataifa.” (Ufunuo 22:2b, NW) Hii “miti ya uhai” lazima pia iwe picha ya uandalizi wa Yehova kwa ajili ya kutoa uhai wa milele kwa aina ya binadamu tiifu.

      25. Ni uandalizi gani ulio tele ambao Yehova hufanyia binadamu waitikivu katika Paradiso ya tufe lote?

      25 Lo! ni uandalizi tele kama nini ambao Yehova anafanyia binadamu waitikivu! Si kwamba wanaweza kushiriki tu hayo maji ya uhai yenye kuburudisha bali waweza wakatunda kutoka miti hiyo namna namna yenye kuendelea ya matunda yenye kudumisha uhai. Oh, laiti wazazi wetu wa kwanza wangalitosheka na uandalizi unaofanana na huu ‘wenye kutamanika’ katika Paradiso ya Edeni! (Mwanzo 2:9) Lakini sasa Paradiso ya tufe lote ipo hapa, na Yehova hata hufanya uandalizi kupitia majani ya miti hiyo ya ufananisho kwa ajili ya “kuponeshwa kwa mataifa.”c Ukiwa wa hali ya juu zaidi kuliko dawa yoyote, ya miti-shamba au nyingineyo, ambayo hutolewa leo, utumizi wenye kutuliza wa majani hayo ya ufananisho utainua aina ya binadamu yenye kuitikadi kwenye ukamilifu wa kiroho na kimwili.

      26. Yamkini pia miti ya uhai inatia ndani nini, na kwa nini?

      26 Miti hiyo, ikiwa inatiliwa maji vizuri na mto, huenda kwa kuongezea ikatia ndani washiriki 144,000 wa mke wa Mwana-Kondoo. Wanapokuwa duniani hao pia wanakunywa kutokana na uandalizi wa Mungu kwa ajili ya uhai kupitia Yesu Kristo. Ndugu hao za Yesu waliozaliwa kwa roho wanaitwa kiunabii “miti mikubwa ya uadilifu.” (Isaya 61:1-3, NW; Ufunuo 21:6) Tayari wao wamefanyiza tunda jingi la kiroho kwa sifa ya Yehova. (Mathayo 21:43) Na wakati wa Utawala wa Miaka Elfu, watashiriki sehemu ya kutoa maandalizi ya ukombozi ambayo yatatumika kwa “kuponeshwa kwa mataifa” dhambi na kifo.—Linga 1 Yohana 1:7.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki