Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Tauni za Yehova juu ya Jumuiya ya Wakristo
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 29. Ni nini kinachotimiza mfananisho wa “nyota kubwa yenye kuwaka kama taa,” na kwa nini?

      29 Sisi tumekwisha kutana na mfananisho wa nyota katika jumbe za Yesu kwa yale makundi saba, ambazo katika hizo zile nyota saba hufananisha wale wazee katika makundi.b (Ufunuo 1:20) “Nyota” zilizopakwa mafuta, pamoja na wengine wote wa wapakwa-mafuta, wanakaa katika mahali pa kimbingu katika maana ya kiroho kutoka wakati ambao wao wanatiwa muhuri kwa roho takatifu hiyo ikiwa dalili ya urithi wao wa kimbingu. (Waefeso 2:6, 7) Hata hivyo, mtume Paulo alionya kwamba kutoka miongoni mwa hao wenye mfano wa nyota wangekuja waasi-imani, wanafaraka, ambao wangeongoza kundi vibaya. (Matendo 20:29, 30) Utoaminifu kama huo ungetokeza uasi-imani mkubwa, na hao wazee walioanguka wangekuja kuwa jumuiya ya “mtu wa kuasi” ambaye angejiinua mwenyewe kwenye cheo kama cha Mungu miongoni mwa aina ya binadamu. (2 Wathesalonike 2:3, 4) Maonyo ya Paulo yalitimizwa wakati viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo walipotokea katika ulimwengu. Kikundi hiki kinawakilishwa vizuri na ule ufananisho wa “nyota moja kubwa ikiwaka kama taa.”

  • Tauni za Yehova juu ya Jumuiya ya Wakristo
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • b Ingawa nyota saba katika mkono wa kulia wa Yesu ni picha ya waangalizi waliopakwa mafuta katika kundi la Kikristo, walio wazee katika makundi 100,000 hivi katika ulimwengu leo ni wale wa umati mkubwa. (Ufunuo 1:16; 7:9) Cheo chao ni nini? Kwa kuwa wao hupokea kuwekwa kwao kwa njia ya roho takatifu kupitia jamii iliyopakwa mafuta ya mtumwa mwaminifu na mwenye uangalifu, hawa wanaweza kusemwa kuwa wako chini ya mkono wa kulia wenye udhibiti wa Yesu kwani wao pia ni wachungaji walio chini yake. (Isaya 61:5, 6; Matendo 20:28) Wao huunga mkono “nyota saba” katika maana ya kwamba wao hutumikia mahali ambako ndugu waliopakwa mafuta wenye kustahili hawapatikani.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki