Wimbo Na. 116
Nuru Inazidi Kuongezeka
Makala Iliyochapishwa
1. Kale manabii walitabiri
Kristo tumaini la wote.
Na masihi aliyeahidiwa,
Kuwakomboa wanadamu.
Sasa Yesu Kristo anatawala.
Ishara zinaonyesha.
Tuna pendeleo kujua hayo,
Malaika huchungulia!
(KORASI)
Nuru inazidi kung’aa;
Twatembea kwenye nuru.
Tazama afanyayo Mungu;
Njiani atuongoza.
2. Tumepewa mutumwa mwaminifu,
Anayetulisha chakula.
Nuru ya Kweli inaongezeka,
Na inachochea mioyo.
Nayo njia yaonekana wazi.
Twatembea kwenye nuru.
Asante Yehova! Chanzo cha kweli,
Asante kwa kutuongoza.
(KORASI)
Nuru inazidi kung’aa;
Twatembea kwenye nuru.
Tazama afanyayo Mungu;
Njiani atuongoza.
(Ona pia Rom. 8:22; 1 Kor. 2:10; 1 Pet. 1:12.)