Wimbo Na. 101
Kutangaza Ukweli wa Ufalme
Makala Iliyochapishwa
1. Hapo mwanzo hatukuwa
Na ujuzi wa Kikristo.
Yehova akatupa,
Ukweli wa Neno Lake.
Tukajua mapenziye,
Kutumika kwa Ufalme,
Kusifu Mungu wetu,
Na jina lake kulitukuza.
Twajulisha watu wote,
Milangoni na njiani.
Ile kweli twafundisha;
Iwekayo watu huru.
Duniani kote kote,
Ibada inapanuka,
Tufanye kazi yake,
Hadi Mungu aseme yatosha.
(Ona pia Yos. 9:9; Isa. 24:15; Yoh. 8:12, 32.)