Wimbo Na. 35
Kuthamini Subira ya Mungu
Makala Iliyochapishwa
1. Yehova u Mungu mukuu,
Wapenda uadilifu.
Nao uovu wazidi,
Twajua wahuzunika.
Watu wadai wakawia.
Wakati wako utafika.
Twakutegemea Wewe.
Asante kwa subira Yako.
2. Kwako miaka elfu moja,
Ni kama siku moja tu.
Siku yako kuu yaja.
Kamwe haitakawia.
Japo uovu wachukia,
Wapenda watu wakitubu.
Twangojea siku yako.
Tukilisifu jina lako.
(Ona pia Luka 15:7; 2 Pet. 3:8, 9.)