Wimbo Na. 62
Sisi Ni wa Nani?
Makala Iliyochapishwa
1. Wewe ni wa nani?
Unamutii nani?
Yule unayemwinamia
Huyo ndiye Mungu wako.
Miungu wawili
Huwezi kuabudu
Na kuwapenda kikamilifu,
Kwa moyo wako wote.
2. Wewe ni wa nani?
Utamutii nani?
Kunaye wa kweli na mwongo.
Utaamua mwenyewe.
Je, ni Kaisari
Utakayemutii?
Ama Yehova Mungu wa kweli
Na kumutumikia?
3. Mimi ni wa nani?
Yehova nitatii.
Nitamutumikia huyo
Niweke nadhiri yangu.
Alininunua
Sitaabudu watu.
Nimekombolewa kwa Mwanaye;
Nitamusifu Yeye.
(Ona pia Yos. 24:15; Zab. 116:14, 18; 2 Tim. 2:19.)