Wimbo Na. 135
Kuvumilia Mpaka Mwisho
Makala Iliyochapishwa
1. Kwa kuwa tuna ahadi,
Piga moyo konde.
Mambo uliyojifunza,
Ni kweli na hakika.
Uwe imara katika
Imani takatifu.
Dumisha utimilifu
Unapojaribiwa.
2. Usipoteze upendo
Wako wa mwanzoni.
Licha ya kujaribiwa,
Uvumilie yote.
Hata nini kikupate,
Usiogope kamwe.
Yehova atakulinda,
Yu karibu na wewe.
3. Watakaovumilia
Wataokolewa.
Majina yako katika
Kitabu cha uzima.
Basi na tuazimie
Kuitimiza kazi.
Ndipo tupate kibali,
Chake Yehova Mungu.
(Ona pia Ebr. 6:19; Yak. 1:4; 2 Pet. 3:12; Ufu. 2:4.)