Maswali Kutoka kwa Wasomaji
◼ Je! Yehova na Kristo ndio wanaomaanishwa kwenye Mithali 30:4, inayouliza: “Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe?“
Mstari huu unaonyesha wazi jinsi mwanadamu alivyopungukiwa akilinganishwa na Aliye Juu Zaidi Sana. Maswali yao yasiyotaka majibu yangeweza kuulizwa kuhusu mwanadamu ye yote, lakini maswali haya yanapaswa yamwongo-ze mtu mwenye kufikiri kwa Muumba.
Mwandikaji Aguri aliuliza hivi: “Ni nani aliyepanda mbinguni na kushuka chini? Ni nani aliyekamata upepo kwa makonzi yake? Ni nani aliyeyafunga maji ndani ya nguo yake? Ni nani aliyefanya imara ncha zote za nchi? Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe, kama wajua?“—Mithali 30:1, 4.
Hakuna binadamu asiyekamilika ambaye amepaa mbinguni na kurudi akiwa mwenye kujua yote; wala hakuna binadamu ye yote mwenye uwezo wa kuongoza upepo, bahari, au nguvu za kijeolojia zinazounda dunia. Basi, Aguri, ni kana kwamba aliuliza, ʼJe! wewe unajua jina, na ukoo wa mwanadamu ye yote ambaye amefanya mambo haya?ʼ Ni lazima sisi tujibu la. —Linganisha Ayubu 38:1-42:3; Isaya 40:12-14; Yeremia 23:18; 1 Wakorintho 2:16.
Hivyo, lazima tuangalie nje ya ulimwengu wa kibinadamu iii kupata mmoja aliye na uweza upitao wa kibinadamu wa kuongoza nguvu za asili. Ingawa hivyo, sisi hatuwezi kujifunza habari zake kwa kutazama tu mambo yake aliyotimiza. (Warumi 1:20) Sababu ni kwamba, yeye ni kana kwamba, ameshuka akiwa na habari juu yake mwenyewe na matendo yake. Yeye ameandaa habari iliyo wazi. Yeye alifanya hilo, kwa mfano, wakati ʼaliposhukaʼ iii ampe Musa sheria juu ya Mlima Sinai. (Kutoka 19:20; Waebrania 2:2) Pia yeye amesaidia watumishi wake wathamini jina lake lenye maana, Yehova. (Kutoka 3:13, 14; 6:3) Baadaye, yeye alimtambulisha Mwanaye, aliyepewa jina Yesu na ambaye alishuka kihalisi kutoka mbinguni akiwa na habari zaidi juu ya Muumba.—Yohana 1:1-3, 14, 18.
Hilo lapaswa kusaidia sisi sote tukate maneno fulani mbalimbali: Kama vile Aguri, sisi hatuwezi kupata hekima ya kweli kwa njia zetu wenyewe. (Mithali 30:2, 3) Na sisi hatuwezi kutaja binadamu ye yote aliye na uwezo wa hali ya juu sana au maarifa. Hivyo, inatupasa kwa unyenyekevu tumtegemee Yeye aliye na uwezo wa kutuandalia hekima tunayohltaji. Huyo ni Aliye Mtakatifu Zaidi Sana, ambaye jina lake tunaweza kujua na ambaye Mwanaye amekufa ili tuweze kukombolewa na kupata uzima wa milele.—Mathayo 20:28.