Wimbo Na. 120
Sikiliza, Tii, Upate Baraka
Makala Iliyochapishwa
1. Kristo Yesu tukimusikiliza,
Na kufanya aliyoagiza,
Tutapata furaha na fanaka,
Kwa kutii tupate baraka.
(KORASI)
Tii ubarikiwe.
Mungu musikilize.
Nawe utakuwa na furaha.
Sikiliza, utii.
2. Maisha yetu ni kama majengo.
Kwenye mwamba twaweza kujenga.
Tumutii Kristo Yesu Kuhani,
Tuwe na kusudi maishani.
(KORASI)
Tii ubarikiwe.
Mungu musikilize.
Nawe utakuwa na furaha.
Sikiliza, utii.
3. Kama miti kando ya maji mengi,
Izaavyo matunda kwa wingi.
Tukitii Mungu kama wanaye,
Uzima milele hatimaye.
(KORASI)
Tii ubarikiwe.
Mungu musikilize.
Nawe utakuwa na furaha.
Sikiliza, utii.
(Ona pia Kum. 28:2; Zab. 1:3; Met. 10:22; Mt. 7:24-27.)