Wimbo Na. 129
Kushikilia Tumaini Letu
Makala Iliyochapishwa
1. Kwa karne nyingi watu wako gizani.
Kazi zao ubatili mutupu.
Inazidi kuonekana wazi:
Kujiokoa hawawezi.
(KORASI)
Mwimbieni na kushangilia!
Ufalme wake unakaribia.
Uovu ataufutilia;
Tumaini letu twashikilia.
2. ‘Siku ya Mungu iko karibu sana!’
Tusilie, ‘Jamani hata lini?’
Karibuni tutapata uhuru.
Yehova Mungu musifuni.
(KORASI)
Mwimbieni na kushangilia!
Ufalme wake unakaribia.
Uovu ataufutilia;
Tumaini letu twashikilia.
(Ona pia Hab. 1:2, 3; Zab. 27:14; Yoe. 2:1; Rom. 8:22.)