Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w15 10/1 uku. 9
  • Je, Wajua?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Wajua?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
  • Habari Zinazolingana
  • Herode Mkuu—Mjenzi Stadi
    Amkeni!—2009
  • “Siku za Mfalme Herode”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Mauaji Kwenye Sherehe ya Sikukuu ya Kuzaliwa
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • “Neno la Yehova Likazidi Kukua”
    “Kutoa Ushahidi Kamili” Kuhusu Ufalme wa Mungu
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
w15 10/1 uku. 9

JE, WAJUA?

Herode alikabili changamoto gani alipokuwa akijenga hekalu la Yerusalemu?

Mwanzoni, Sulemani alijenga hekalu la Yerusalemu juu ya mlima na akaagiza kuta zijengwe upande wa mashariki na magharibi ili kutengeneza mfululizo wa ngazi pana kuzunguka hekalu hilo. Herode alitaka kujenga hekalu zuri zaidi ya lile la Sulemani, kwa hiyo akaanza kurekebisha na kupanua hekalu lililokuwapo.

Mchoro unaoonyesha hekalu na ukuta uliozunguka

Mafundi wa Herode walipanua eneo tambarare kaskazini mwa hekalu ili kuongeza mfululizo wa ngazi pana katika eneo hilo. Eneo tambarare lenye upana wa meta 32 liliongezwa upande wa kusini. Walitengeneza safu ya vyumba vya mawe na ukuta mnene kuzunguka vyumba hivyo. Katika sehemu fulani, ukuta huo ulifikia urefu wa meta 50.

Herode alijitahidi asiwakwaze Wayahudi au kuvuruga shughuli zilizokuwa zikiendelea hekaluni. Mwanahistoria Myahudi Yosefo anasema kwamba Herode aliwafundisha makuhani wa Kiyahudi kuchonga mawe na useremala kwa kuwa wao tu ndio walioruhusiwa kuingia katika sehemu takatifu za hekalu.

Herode alikufa kabla ya mradi huo kukamilika. Kufikia mwaka wa 30 W.K., hekalu hilo lilikuwa limejengwa kwa miaka 46. (Yohana 2:20) Kitukuu cha Herode, Agripa wa Pili, alimaliza kazi hiyo katikati ya karne ya kwanza W.K.

Kwa nini watu wa Malta walifikiri kwamba mtume Paulo alikuwa muuaji?

Mungu wa kike wa haki akimpiga mungu wa kike wa ukosefu wa haki

Mungu wa kike wa haki (Kushoto) akimpiga mungu wa kike wa ukosefu wa haki

Huenda baadhi ya watu wa Malta waliathiriwa na mafundisho ya dini ya Wagiriki. Fikiria kilichotokea baada ya meli aliyopanda Paulo kuvunjika akiwa Malta, kama inavyosimuliwa katika kitabu cha Matendo. Mtume huyo alipokusanya kuni na kuziweka juu ya moto ili kuwapasha joto abiria wenzake, nyoka-kipiri alijifunga kwenye mkono wake. Walipoona hilo, wenyeji wa kisiwa hicho walisema hivi: “Hakika mtu huyu ni muuaji, na ingawa alifika mahali salama kutoka baharini, haki yenye kudai kisasi haikumruhusu aendelee kuishi.”​—Matendo 28:4.

Neno la Kigiriki “Haki” lililotumika hapa ni “di’ke.” Neno hilo linaweza kumaanisha haki katika hali isiyo halisi. Hata hivyo, kulingana na hekaya za Kigiriki, mungu wa kike wa haki aliitwa Dike. Ilidhaniwa kwamba alisimamia mambo yote ya wanadamu na alitoa taarifa kwa Zeu kuhusu ukosefu wowote wa haki ambao haukugunduliwa ili wenye makosa waadhibiwe. Hivyo, kulingana na chanzo kimoja, huenda wenyeji wa Malta walifikiri hivi: “Ingawa Paulo hakufa baharini, ametiwa alama na sasa anahukumiwa na mungu wa kike Dike . . . kupitia nyoka kipiri.” Watu walibadili maoni yao walipoona Paulo yuko hai.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki