Wimbo 168
Kumkubali Mfalme Mpya wa Dunia
1. Ona kule, mbali kule
Kinifurahishacho
—Jeshi lake Yehova kwa
Umoja linasonga.
Kofia zao zang’aa,
Ujinga wazikimbia.
Sauti wanazipaza:
“Kristo anatawala.”
(Korasi)
2. Kristo Yesu aongoza;
Yeye wamufuata.
Asema, na wanatii
Hawaoni huzuni.
Upanga, Neno la Mungu.
Nyayo zinavyo viatu
Vya Injili. Wafuata;
Bwana hadi na kifo.
(Korasi)
3. Tazama saa yafika
Ya Kristo kutawala.
Adui kuramba vumbi;
Wagwaye mbele yake.
Mungu amusaidia.
Tarumbeta inapigwa.
Watawala, mahakimu,
Tiini Kristo Yesu.
(KORASI)
Busuni Mwana,
Asikasirike Mungu, mufe.
Wenye furaha wenye
kumutumaini!