Wimbo 193
Hubiri “Habari Njema Hizi za Ufalme”!
1. Lazima habari njema zitangazwe,
Ushuhuda kwa mataifa.
Jina zuri la Yehova lisifiwe,
Na kabla halijatetewa.
(Korasi)
2. Siku mbaya na tununue wakati
Toka anasa za dunia.
Ufalme kwanza na kumutumikia,
Tupate hazina milele.
(Korasi)
3. Usiwe na hofu unapohubiri,
Japo upate upinzani.
Kwa fadhili na busara endelea;
Hubiri kwa uaminifu.
(KORASI)
Hubiri habari njema.
Uwasaidie wapole.
Wakubwa kwa wadogo wawe upande,
wa Mungu watakase jina.