Wimbo 29
Haya Mbele, Enyi Mashahidi!
1. Muda wa mwisho wanaazimia
Watumishi injili kupigania.
Shetani akiwaringia,
Nguvu Mungu awapatia.
(Korasi)
2. Haki, ukweli, zimewekwa kando.
Jina la Yah linapigwa marufuku.
Yarudishwe mahali pake
Wakristo wanaoangaza.
(Korasi)
3. Askari wa Mungu hawali raha.
Na ulimwengu hawataupendeza;
Huwa bila doa daima,
Ni wakamilifu daima.
(KORASI)
Haya songeni mbele, E Mashahidi!
Furahi kushiriki kazi ya Mungu!
Tangaza Mufumo Mupya karibu,
Na baraka tele zaja nao!