Wimbo 111
Nuru Yazidi Kung’aa
1. Nuru ya Neno la Mungu yazidi
Kung’aa na kuzidi Siku karibu.
Na Yehova, anafunua kweli;
Anatusihi hivi: ‘Tega, sikio.’
Hatumo gerezani mwa
Dini ile ya uwongo.
Kweli zipo.
“Siku ya Bwana,”
Ona nuru kama nuru ya jua,
Kuwapa waadilifu mwangaza mwingi,
Nuru ya Mungu.
2. Nuru kubwa inang’aa njiani.
Yaletwa na Yehova na kwa upendo.
Afanya kufahamu kweli wazi;
Anafinyanga watu na kweli zake
Kwa kutokukamilika
Huenda tukakosea;
Na ukweli
unasafisha.
Mungu wetu anatuangazia.
Bado anatoa nuru yake tukufu,
Nuru zaidi.
3. Nuru nyingi inatuangazia
kama nuru ya jua la adhuhuri.
Yehova ni nuru atuangaza;
’Angaza njia yetu, tusiogope.
Tusishuku kamwe wala
Kuwa na haraka kamwe.
Shika njia
usiiache.
Kuna nuru na itaongezeka.
Waadilifu Wanafurahia nuru.
Nuru zaidi.