Wimbo 63
Acheni Nuru Ing’ae
1. Mungu aagiza
Nuru ing’ae
Giza ifukuze,
litokomee.
Hekalu kwa Mungu
’Toka umeme,
Ili tuongozwe
Kwa nuru yake.
2. Sisi twaeneza
Habari njema
Tukiwafariji
Waombolezi,
Nguvu zetu zote
za kushuhudu
Zatoka kwa Mungu.
Mwenye agizo.
3. Kufanya kazi kwa
Imani yote,
Kuwa imara, na
Wakamilifu.
Sisi watu wake,
Tunatangaza
Utukufu wa jina
Lake safi.