Wimbo 167
Shukrani kwa Mpaji wa Uzima
1. Asante, Mungu, Baba Yehova.
Tunakusifu kwa moyo wetu.
Twafuata hatua za Yesu,
Tunainua mikono yetu.
2. Twafurahi Mwenye Enzi Kuu;
Mbingu na dunia zakutii.
Tunakupa vitu vyetu vyote,
Kwayo ibada, na kukutii.
3. Umeuweka Ufalme wako;
Sisi tuna amani na wewe.
Twakuomba hekima daima,
Tukuheshimu ustahilivyo.
4. Kwa shukurani tukutumikie,
Julisha wema na Neno lako.
Zibariki jitihada zetu,
Na roho yako itupe nguvu.