Wimbo 209
Fuateni Mfalme Shujaa wa Vita!
1. Tuna wimbo wa kusifu Yehova;
Tuna wimbo wa kumutukuza.
Tuna ujumbe wote wasikie
Agizo la kusema habari.
(Korasi)
2. Mashujaa ingieni vitani
Fwateni Kapteni wa taifa;
Twaeni ngao, imani, upanga,
Vaeni kofia ya wokovu.
(Korasi)
3. Si kwa uwezo wetu tunaweza;
Kushinda vita si kwetu sisi.
Kwa nguvu zake Mungu tutashinda,
Kutukuza jina la Yehova.
(KORASI)
Tusonge! (Mbele!)
Bila woga! (Bila woga!)
Kama jeshi twendeni
Tukapige adui;
Fuateni Shujaa ’siyeshindwa.
Fuateni, tutashinda!