Wimbo 135
Yehova, Kao Letu
1. Yah umekuwa kao letu
Vizazi vyote zamani.
Milima usijaiumba
U mutukufu milele.
Wewe u Mungu wa milele;
U yuleyule daima.
‘Tujapofanywa vumbi’ nawe,
Pendo lilituokoa.
2. Miaka elfu ikipita,
Kwako ni kama jana tu.
Kucha mutu yuatokeza
Kama nyasi, anyauka.
Miaka yetu ni sabini,
Themanini, tukiweza;
Yajikaza kwenye taabu,
Nayo ni ya kuumiza.
3. Tufunze kuhesabu siku,
Tufurahie zaidi.
Twakaza moyo hekimani,
Vinywa vyetu vyakusifu.
Uzuri wako Yehova ’we,
Wape watumishi wako.
Ithibitishe kazi yetu;
Thibitisha utendaji.