Wimbo 10
Iweni Imara, Bila Kuondoleka!
1. “Siku za mwisho” zinapokoma,
Utumishini twajitumika.
Twataka tuwe imara sana,
Kutumikia Mungu.
(Korasi)
2. Mikazo ya mufumo yazidi.
Akili timamu tuzitunze.
Tukiwa imara kwake Mungu,
Atatusalimisha.
(Korasi)
3. Tutumikie Mungu kwa nguvu.
Tuitunze njozi iwe wazi.
Twendelee na Habari Njema.
Siku hizo kupita.
(KORASI)
Imara sote tuwe; Mbali na ulimwengu
Tukilishwa kweli na ukamilifu.