Wimbo 164
Watoto—Zawadi Bora za Kutoka kwa Mungu
1. Watoto zawadi toka kwa
Mungu, ni mali kufundisha.
Tuwalenge kama mishale
Ya shujaa kwenye shabaha.
Hao zawadi;
Mungu asema:
‘Tumia fimbo’ Kwa upendo.
Toa sala uwazoeze.
2. Kujua moyo wa kijana,
Inataka ustadi mwingi.
Twaanza mapema kufunza
Ukweli wakiwa wachanga.
Tuguse moyo;
Na tukiwahi.
Tuombe Mungu musaada,
Tutumie maneno yake.
3. Kupashana habari nao,
Watajiona wako huru
Kusema ya moyoni mwao;
Tutakuwa rafiki zao.
Usikemee.
Pasha habari.
Sisi tusiwe na lawama
Tulengapo mishale hiyo.
4. Watoto ni urithi wetu
—Bali ni mali yake Mungu.
Uzao uletao mema
Wakijua jema na baya.
Twatumaini
Watajifunza.
Tumai kulipwa na Mungu.
Tusifu Mungu na watoto.