Wimbo 107
Mwimbie Yehova Sifa kwa Ushujaa!
1. Tumusifu Yah kwa ushujaa,
Kwa nguvu zake tunashinda.
Adui wasituogopeshe.
Tusiwahofu. Twende mbele.
(Korasi)
2. Tumusifu Yah kwa ushujaa
Tuonye wote wasikie;
Mufalme ataua waovu,
Dini za uwongo kuisha.
(Korasi)
3. Tumusifu Yah kwa ushujaa,
Na wanyofu tuwafundishe,
Vilevile na wanyenyekevu,
Mapenzi yake watimize.
(KORASI)
Tangaza kote habari njema.
Wasaidie wawe wakifu.
Tumusifu Yah kwa ushujaa,
Tukuze jina lake kuu.