Wimbo 160
Kutembea kwa Ukamilifu
1. Nihukumu mimi, E Yehova.
Nimekutumai, wewe sana sana.
Nichunguze na unijaribu;
Takasa akili, moyo, nibariki.
(Korasi)
2. Sikai na waovu waongo.
Waufanyiao ukweli utani.
Usitwae uhai wangu na
Waovu wapenda rushwa na ugomvi.
(Korasi)
3. Nimependa kao la nyumbako.
Nitoe ibada; yako safi sana.
Nizunguke madhabahu yako
Nihubiri kote shukurani zangu.
(KORASI)
Ila mimi, Nitaazimia
kuenda milele kwa ukamilifu.