Wimbo 62
Wenye Furaha, Warehemifu!
1. Wa furaha wa rehema!
Mungu aona wazuri.
Wenye haki waambiwa
Mungu anawarehemu.
Zilionyeshwa Kalvari,
Ukombozi ’katolewa.
Mungu huwapa wapole,
Ajua sisi dhaifu.
2. Wa rehema wa baraka;
Dhambi anawasamehe.
Wanafaidika kwani
Yesu anawatetea.
Wanashiriki rehema,
Kwa kulihubiri Neno,
Kwa kusema: “Furahini
Kwani Ufalme u hapa.”
3. Wa rehema hawahofu
Mahakama yake Mungu;
Watajulishwa rehema,
Kwa kuwa wanarehemu.
Na tuwe wenye rehema
Tuonyeshe sifa hiyo.
Kutumia kila pindi
Kumwiga Mungu Mbinguni.
(UBETI WA MWISHO)
Wa furaha wa rehema!
Mungu aona wazuri.