Wimbo 147
Hazina Zisizoshindwa Kamwe
1. Baba yetu tunasema asante
Tunafahamu ukweli!
Ni pendeleo kuhubiri ’Falme
Kujua uko karibu.
2. Hekima na haki, nguvu, upendo
Jinsi zatusisimua.
Tunafurahia kuwa na Yesu,
Kama Muokozi wetu.
3. Urafiki na wewe ni baraka.
Tutamani nini tena?
Fadhili zako zaleta amani
Nasi tunazitamani.
4. Tuna sababu za kukushukuru;
Neno lako litadumu.
Unawapa watu wako baraka.
Ni hazina ya kudumu.