Wimbo 153
Yehova, Mungu wa Wokovu Wetu
1. Bwana Mungu kule juu,
Tusamehe dhambi zetu.
Tulizaliwa dhambini
Hatukuwa na ukweli.
Tafadhali tuokoe.
Tuongoze, E Yehova.
Utupe kibali chako,
Wokovu wako tuimbe.
Wokovu wako tuimbe.
2. Tumekusanywa zizini
Mwako, tukiwa kondoo.
Wokovu wapatikana
Kwa watu wa duniani.
Twajua amani yako
Unayowapa wapole.
Hekima kukuogopa;
Wokovu uko karibu.
Wokovu uko karibu.
3. Kweli zako zachipuka!
Tuna sababu ya shangwe.
Leo twaona ajabu,
Sababu Yesu Mufalme.
Ufalme unatawala,
Amani inasitawi.
Na tuitangaze kote.
Wokovu wetu watoa.
Wokovu wetu watoa.