Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 3/95 uku. 3
  • Tukio la Maana Zaidi Katika Historia ya Binadamu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Tukio la Maana Zaidi Katika Historia ya Binadamu
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Kuadhimisha Kifo Kitoacho Tumaini la Uhai wa Milele
    Huduma Yetu ya Ufalme—1993
  • Kwa Nini Tunaadhimisha Mlo wa Jioni wa Bwana?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
  • Mlo wa Jioni wa Bwana Huadhimishwaje?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Uthamini Wako kwa Kifo cha Kristo
    Huduma Yetu ya Ufalme—1992
Pata Habari Zaidi
Huduma Yetu ya Ufalme—1995
km 3/95 uku. 3

Tukio la Maana Zaidi Katika Historia ya Binadamu

1 Yesu alikuja duniani kwa mwelekezo wa Baba yake ili kushuhudia kweli ambayo ingetuongoza kwenye uhai wa milele. (Yn. 18:37) Uaminifu wake hadi kifo ulimletea Yehova heshima, ukatakasa jina la Mungu, na kuandaa fidia. (Yn. 17:4, 6) Hilo ndilo lilifanya kifo cha Yesu kiwe tukio la maana zaidi katika historia yote ya binadamu.

2 Tangu kuumbwa kwa Adamu, kumekuwa na watu wakamilifu wawili tu ambao wameishi juu ya dunia hii. Adamu angaliweza kuwaletea wazao wake ambao hawakuwa wamezaliwa bado baraka nzuri ajabu. Badala ya hivyo, yeye aliasi kwa ubinafsi, akiwaletea adhabu ya kuwako kwenye huzuni ambako kungeishia katika kifo. Yesu alipokuja, alionyesha uaminifu mshikamanifu na utii mkamilifu, akifungua njia ya fursa ya kupata uhai wa milele kwa wote wanaodhihirisha imani.—Yn. 3:16; Rum. 5:12.

3 Hakuna tukio jingine lolote liwezalo kulingana na kifo cha Yesu cha kidhabihu. Kilibadili mwendo wa historia ya binadamu. Kiliandaa msingi wa kufufua mabilioni ya watu kutoka kwa wafu. Kiliwekea msingi Ufalme wa milele ambao ungeleta mwisho wa uovu na kufanya dunia iwe paradiso. Hatimaye kitaweka huru wanadamu wote kutoka katika kila namna ya uonevu na utumwa.—Zab. 37:11; Mdo. 24:15; Rum. 8:21, 22.

4 Hayo yote yatusaidia tuthamini ni kwa nini Yesu aliwaagiza wanafunzi wake wakumbuke kifo chake kwa adhimisho la Ukumbusho kila mwaka. (Luka 22:19) Kwa kung’amua umaana wacho, sisi twatazamia kukutana na makutaniko ya Mashahidi wa Yehova ulimwenguni pote baada ya jua kushuka mnamo Ijumaa, Aprili 14. Kabla ya wakati huo, ingekuwa vizuri kusoma pamoja tukiwa familia masimulizi ya Biblia juu ya siku za mwisho za Yesu akiwa duniani na msimamo wake wenye moyo mkuu kwa ajili ya kweli. (Mafungu yaliyopendekezwa yameonyeshwa ama katika kalenda yetu ya 1995, Aprili 9-14 ama katika Kuyachunguza Maandiko Kila Siku—1995.) Yeye alituwekea kigezo cha ujitoaji kwa Muumba wetu. (1 Pet. 2:21) Na tufanye yote tuwezavyo kualika marafiki na familia zetu, na pia wanafunzi wa Biblia na watu wengine wenye kupendezwa, kwenye kusanyiko hili la maana. Eleza kabla ya wakati yale yatakayotendeka na umaana wa mifano.—1 Kor. 11:23-26.

5 Wazee wapaswa kupanga kimbele ifaavyo ili kuhakikisha kwamba Jumba la Ufalme liko nadhifu na safi. Mipango yapasa kufanywa kwa mtu fulani kupata mifano. Kutolewa kwa mifano kwapasa kupangwe vizuri. Madokezo yenye kusaidia ya jinsi tuwezavyo kuonyesha staha kwa ajili ya Mlo wa Jioni wa Bwana yalitolewa katika Mnara wa Mlinzi la Machi 1, 1985, ukurasa 17. Ingefaa sana kwa kutaniko kupangia utendaji mwingi uliopanuka wa utumishi wa shambani wakati wa siku kadhaa kabla ya adhimisho na pia siku chache baada yalo.

6 Mwaka uliopita, jumla ya watu 12,288,917 walihudhuria ulimwenguni pote ukumbusho wa tukio hili la maana. Kwa kuwa ni siku ya maana zaidi katika kalenda yetu, sisi sote twapaswa kuwapo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki