Wimbo 3
Kupata Ushindi Juu ya Ulimwengu
1. Tusongapo kwa ushindi
Kwa nguvu za Yehova,
Yeye hutupa ushindi
Katika vita vyema.
Tunachukiwa na watu
Tuhubiripo Neno.
Tukihakiki kushinda,
Tutasonga tu mbele.
2. Tutazipata taabu.
Twajua jambo hilo.
“Jipeni moyo” tu! Yesu
Kasema. ‘Tawalinda.’
Tunaweza kushinda tu,
Vita si yetu sisi.
Yehova apiga vita;
Moto wala adui.
3. Twaushinda ulimwengu
Kwa kuamini Yesu.
Ufalme upo, na Yesu
Atumia upanga.
Na Yesu aliushinda
Ulimwengu, na sisi.
Pia tutaushinda, kwa
Kutumaini Mungu.